Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA–, serikali ya Iraq imetangaza rasmi taratibu za kuingia na kutoka nchini kwa raia wa kigeni na wahamiaji wanaotarajiwa kushiriki katika ibada ya Arubaini ya Imam Hussein (as).
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mahujaji (mazuwwari) wote wanaoelekea kuzitembelea haram takatifu za Imam Husayn (as) na Abu al-Fadhl al-Abbas (as) katika mji wa Karbala wanapaswa kutumia vituo vya mipakani vilivyotengwa kwa ajili ya kuingia na kutoka nchini, kwa kuzingatia maelekezo yaliyowekwa na mamlaka husika.
Hatua hiyo inalenga kurahisisha usafiri wa mamilioni ya waumini wanaotarajiwa kuwasili Iraq kutoka mataifa mbalimbali duniani, pamoja na kuimarisha usalama, uratibu wa huduma na usimamizi wa shughuli za hija ya Arubaini.
Kila mwaka, ibada ya Arubaini ya Imam Hussein (as) hukusanya mamilioni ya mahujaji (mazuwwari)kutoka pembe mbalimbali za dunia, na kuwa moja ya mikusanyiko mikubwa zaidi ya kidini duniani, huku waumini wakitembea kwa miguu kuelekea Karbala kuadhimisha kumbukumbu ya siku ya arobaini tangu kuuawa shahidi kwa Imam Husayn (as) na wenzake katika tukio la Karbala.
Iraq yatangaza vituo vya mipakani kwa raia wa kigeni na wahamiaji watakaoshiriki Arubaini ya Imam Husayn (as)
13 Julai 2026 - 23:29
News ID: 1839874
Serikali ya Iraq imetangaza taratibu za kuingia na kutoka nchini kupitia vituo maalumu vya mipakani kwa raia wa kigeni na wahamiaji wanaokusudia kushiriki ibada ya Arubaini ya Imam Husayn (as) katika miji mitakatifu ya Najaf na Karbala.
Your Comment